Tuesday, October 25, 2011

DOCTOR WA MICHAEL JACKSON.....NGOMA NGUMU!

          
                                       DOCTOR CONRAD MURRAY
Kesi inayomkabili Doctor wa Michael Jackson,Conrad Murray ya kusababisha kifo cha MJ,inaenedelea lakini inaelekea jumba kumuangukia baada ya kudaiwa kukosea matibabu aliyoyatoa
Inasemekana Dr Murray amefanya makosa mengi ikiwemo kumpa dawa aina ya Propofol,iliyodaiwa kuwa inanguvu na haitumiki kwa kutibu insomnia

MICHAEL JOSEPH JACKSON (29 AUG,1958 - 25 JUNE,2009)
Ilifunguliwa kuwa ni kweli Michael Jackson aliomba msaada kwa doctor wake,Conrad Murray lakini alitakiwa awe makini kwenye kazi yake na kitendo cha Dr Murray kuchelewa kupiga namba 911 kuomba msaada,anaonekana moja kwa moja kama alikua mzembe ambao huenda ukasababisha kifo cha King of Pop,Michael Joseph Jackson aliyefariki June 25,2009

RAPPERS KANYE WEST NA JAY-Z....WASHITAKIWA....!


SYL JOHNSON - AMERICAN SOUL LEGEND
Rappers,Jay Z na Kanye West wameshitakiwa kwa ku-sample moja ya nyimbo zilizomo kwenye collabo album yao ya,Watch The Throne
....KANYE WEST vs JAY Z....
Syl Johnson ambaye ni mwanamuziki wa Soul wa Marekani,amefungua mashitaka kwenye mahakama ya Illinois,akidai kuwa Jay Z na Kanye West wame-sample bila ya ridhaa yake,ngoma yake iitwayo Different Strokes iliyotoka mwaka 1967 na wao kutoa ngoma iitwayo The Joy,na mpaka sasa Syl Johnson hajafunguka kama anadai mkwanja kiasi gani na si Jigga au Kanye au wasemaji wao hawajatoa comment zozote mpaka sasa

....PICHA ZAIDI ZA KIFO CHA MUAMMAR GADDAFI....


....SEHEMU ALIPOJIFICHA PANDE ZA HOMETOWN KWAKE,SIRTE....
....WAASI WAKIMNG'ANGANIA....
....MAITI YAKE....
....BASTOLA YA GADDAFI....FULL GOLD....

....MAN UNITED YAPATA 'KIPIGO CHA ADABU'.....!

                                      
                                                                                               
                
                                           ....MARIO BALOTELI....NDIYE ALIEANZISHA KIPIGO....
Manchester United imepata 'kipigo kikubwa cha adabu' toka February 1955 kwenye Premier League,ikwa ni miaka 56 tangu mabingwa hao wa kihistoria wa Uingereza kupata kipigo kikubwa hasa kwenye Uwanja wa Old Trafford
Kikosi cha Manchester United chini ya kocha Roberto Mancini imeipa kipigo Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson tangu mwaka 1930, baada ya Huddersfield kushinda 6-0 na Newcastle United kushinda 7-4 baada ya siku 4
Mario Balotelli alianza kutupia dakika ya 22 na dk 60,baadaye Sergio Kun-Agüero dk 69 kabla ya Darren Fletcher kurudisha goli moja dk ya 81, na David Silva na Edwin Dzeko kumalizia maumivu.....
....MASHETANI WEKUNDU....MAJI YALIPOZIDI UNGA.....!
....BAADA YA DAKIKA 90....MAN UTD 1 - MAN CITY 6....

CHRIS BROWN vs RIHANNA...KUWANIA TUZO MOJA..!



Artist waliokua wana-share malavidavi Rihanna na Chris Brown wamechaguliwa kugombea category moja kwenye tuzo za Soul Train Awards 2011
    




    
                                                              CHRIS BROWN
Rihana na Chris Brown wanagombania tuzo ya The Best Dance Performance na Rihanna anagombea kupitia track yake ya Only Girl (In The World)/What’s My Name,wakati Chris Brown ameingia na track yake ya She Ain’t You na kufanya awe anagombea category 5 tofauti ikiwemo Song Of The Year na Album Of The Year wakati Artist Beyoncé Knowles aka Mrs Jigga anawania tuzo 4 na tuzo hizo zitatolewa jijini Atlanta-Marekani,tarehe 17 November,2011








                                                     




                                   

Wednesday, October 12, 2011

kelly-rowland amsamehe-dingi-yake.html

                      KELENDRIA TRENE ROWLAND - KELLY ROWLAND
Member wa Zamani wa 'kundi Marehemu' la Destinys Child,Kelly Rowland amefunguka hadharani kuwa yuko tayari kukutana na baba yake baada ya kuchuniana kwa miaka 20 baada dingi yake huo kujaribu kurudi karibu na Kelly Rowland kupitia media
Dingi yake Kelly Rowland Now Lovett mwenye miaka 65,alisepa na kusababisha mtafaruku kwenye familia hasa yeye na mama yake kufukia kutoonana pia na Mama yake Mzazi, Lakini kwa sasa yuko tayari kukutana nae na amemsamehe kwa yote....

rihanna amsanua-boyfee-wake-mpya..

 
                                         ROBYN RIHANNA FENTY
Artist toka Barbados,Robyn Rihanna Fenty amemsanua boyfriend wake mpya jijini London walipokwenda out
DUDLEY O'SHAUGHNESSY - UK BOXER
Rihanna alionekana na Boxer Dudley O’Shaughnessy pande za Mahiki Nightclub baada ya concert yake aliyofanya pande za O2 Arena
....DUDLEY vs RIHANNA....
Mashuhuda wamefunguka kuwa RiRi na Dudley hawakuficha kama wana share 'loveydovey' na walijiachia ile mbaya na imefunguliwa kuwa RiRi alikutana na Dudley wakati wa shooting ya video ya I Found Love mwezi September alipokua Ireland Kaskazini,na Dudley alichaguliwa na Rihanna auze kwenye video hiyo na pia RiRi amemuomba Dudley ampe 'company' kwenye tarehe zilizobaki z

beyonceafunguka-mwezi-wa-kujifungua.

                                                    ....BABY MAMA TO BE....BEYONCE....
Artist na Baby Mama to be,Beyonce amefunguka siku ya kumleta duniani mtoto wake wa kwanza na Rapper Jay-Z baada ay miaka 3 na nusu ya ndoa
....JIGGA vs BEY....
Beyonce alifunguka kwenye interview ya TV ya Australia kuwa anategemea kujifungua mwezi February 2012,na kufunguka zaidi yeye na Jay-Z wamekua pamoja kwa miaka 10 na kumshukuru mungu kwa baraka zake na kufunguka kuwa alikua hana haja ya kuharakisha mambo kwani kwa sasa ana miaka 30 na ni wakati wa yeye kufanya atakacho na ni mwenye furaha maishani

Thursday, October 6, 2011

WYRE.....AGONGA TRACK NA MORGAN HERITAGE....!

 KELVIN WYRE AKA THE LOVE CHILD - KENYAN ARTIST
Reggae na Dancehall artist toka Kenya,Wyre 'The Love Child' kwa sasa amebakisha hatua chache ya kutambulika kuwa anawazimia atrist toka Jamaica baada ya kurekodi track na Reggae brothers Gramps na Peetah Morgan toka kwenye bendi ya Morgan Heritage
GRAMPS MORGAN,WYRE NA PEETAH MORGAN
Gramps na Peetah Morgan walikua nchini Kenya kwa ajili ya shughuli za charity kwenye project iitwayo Give Hope Africa na kugonga ngoma iitwayo Guarantee,inayopata airtime ya kutosha kwenye radio stations ikiwa video bado haijakuwa released
Wyre amesharekodi ngoma na Jamaican Bad Gal,Artist Cecile ya She Say Dat RMX na kwa sasa imechaguliwa kwenye Channel O Music Video Awards-2011 kama The most gifted Ragga Dancehall video na pia Wyre amegonga ngoma na Chege Chigunda toka TMK Wanaume Family inayoitwa Usiniache

jay-z-afunguka sina-beef-na-lil-wayne.

SHAWN COREY CARTER – JAY Z
Jay-Z maefunguka kuwa kwa sasa akili yake iko zaidi kumfikiria mtoto wake mtarajiwa na tour ya joint album yao na Kanye West ya Watch The Throne,tour ambayo inatarajiwa kuanza mwezi ujao na kufunguka kuwa hana mpango wa beef na Lil Wayne
DWAYNE MICHAEL CARTER,JR. - LIL WAYNE
Lil Wayne alimchana Jigga kwenye album yake ya Tha Carter IV kwenye ngoma ya It’s Good featuring Jadakiss na Drake...na verse ilikwenda kama Talkin’ about baby money,I got your baby money,kidnap your bi*ch,get that how much you love your lady money/I know you fake ni**a,press your brakes ni**a/ I’ll take you out,that’s a date,ni**a,raps the Young Money MC....Ikiwa ni jibu la diss verse toka kwenye ngoma ya Jay-Z ya H.A.M,.....I’m like really, half a billi,ni**a really you got baby money/Keep it real with ni**as,ni**as ain’t got my lady money na baadaye H.O.V.A. Kufunguka zaidi kuwa haina haja ya kuwa na beef kwenye Hip-Hop coz That’s sport,that’s rap music,Nothing is going to change but the participants....
JAY-Z vs LIL WAYNE
   

LADY GAGA....USO KWA USO NA RAIS OBAMA....!

                             BARACK HUSSEIN OBAMA - US PRESIDENT



US Prezidaa,Barack Obama alitoa kali baada ya kukutana na Artist Lady Gaga kwenye hafla ya kuchangia fedha ya taasisi ya Human Rights Campaign jijini Washington D.C na alitania kuwa alikua anaogopa kukutana na Msanii mwenye vituko,Lady Gaga
STEFANI JOANNE ANGELINA GERMANOTTA - LADY GAGA
Rais Obama alikuatan an makundi mbali mbali yanayodai haki wakiwemo mashoga na wasagaji,Na baadaye Lady GaGa alitupia kwenye Twitter account kuwa alikua anataka sana kukutana na Barack Obama, baada ya dogo Jamey Rodemeyer toka Williamsville,New York aliyekua ana miaka 14 kujiua baada ya kunyanyapaliwa kwa kua alikua shoga, Lady Gaga alifunguka kuwa nia ya kukutana na Rais Obama ni kushinikiza jamii na kizazi kwa ujumla kuachana na tabia hii,coz yeye peke yake hawezi bali kwa pamoja....

RIHANNA AZINGUA LOCATION YA VIDEO MPYA

 ROBYN RIHANNA FENTY - RIHANNA
Baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la We Found Love,Robyn Rihanna Fenty aka Rihanna amefunguka jina la album yake ya 6
....RIHANNA....ON SET...
Album yake ya 6 itaitwa Talk That Talk na baada ya kutoa first single iitwayo We Found Love amesepea pande za Northern Ireland kwa ajili ya kutengeneza video ya ngoma hiyo na kuleta mtafaruku kutokana na scene aliyotumia wakati wa kufanya video ya We Found Love,baada ya kuonekana akiwa topless na kuzua malamiko toka kwa mkulima mwenye shamba lake lililotumika kama location Alan Graham,aliyempa Rihanna shamba lake la Ngano lililopo pande za Bangor County Down,Belfast
....WE FOUND LOVE...VIDEO MAKING....

Wednesday, October 5, 2011

DU MIMBA YA BEYONCE YAMCHUKIA JAY-Z

 JAY Z vs BEYONCE
Baby Mama mtarajiwa na mke wa Jay-Z,Beyonce ameshaanza 'vituko vya ujauzito' na kufunguka kuwa kwa sasa haipendi kabisa harufu ya husband wake,hip-hopper....Jay-Z
Beyonce alifunguka zaidi alipokua anaitangaza perfume yake ya Pulse nchini Canada,kuwa anamzimia sana Jay-Z,na anapenda harufu ya kila kitu ila kwa sasa haizimii harufu yoyote toka kwa Jigga na kwa sasa haijajulikana mtoto wa 'B' na Hova atakua ni wa jinsia gani na wote wamekua wakiagizia viwalo vya mtoto vya jinsia tofauti....
 









Artist wa Bongo Flava,Naseeb Abdul alifanya 'suprise' pande za Maisha Club kwenye Birthday Party yake pande zile,kwa kumvalisha kitu cha pete ya uchumba,mtu wake Wema Abraham Sepetu (Miss TZ-2006)
....KITU CHA ENGAGEMENT RING AKA PETE YA UCHUMBA....
....Kila la Heri 'bongo celebrity couples'....hope ndoa itafungwa soon na haitakua hadithi njoo,utamu kolea kama....kina flani hivi...!

ARTIST WALIPOFUNIKA....TPF-CONCERT....NAIROBI..!

 





...SHAGGY.....TOKA JAMAICA....
....CABO SNOOP....TOKA ANGOLA....
....FEMALE RAPPER-EVE....TOKA MAREKANI....
....'HOMEBOY' PETER MSECHU....TOKA TANZANIA....
....ALPHA RWIRANGIRA....TOKA RWANDA....
....DAVIS NTARE....TOKA UGANDA....
....JAGUAR....TOKA KENYA....
 










DWAYNE MICHAEL CARTER JR. - LIL WAYNE
Kuna za Chini ya Carpet kuwa Artist wawili toka Young Money Entertainment,Dwayne Michael Carter, Jr. aka Lil Wayne na Onika Tanya Maraj aka Nicky Minaj wametengeneza sex tape ya pamoja
ONIKA TANYA MARAJ - NICKI MINAJ
Mtandao mmoja wa kimbea zaidi duniani,umefunguka kuwa sex tape hiyo imerokodiwa miaka 3 iliyopita hivi,na anaoneka kama mtoto aliyekua na Weezy ni Superbass rapper,Nicki Minaj na kufunguliwa kuwa kwa sasa anatafutwa don mwenye hela ndefu ili auziwe kwa dola 150,000 ili uoneshwe hadharani
LIL WAYNE vs NICKI MINAJ
Lakini mpaka sasa hakuna msemaji wa Nicki Minaj naWeezy kuzungumzia issue hiyo....