Wednesday, November 23, 2011

WEMA SEPETU kwa mara nyingine tena!!!!!!



    

Movie star wa bongo WEMA SEPETU, wife to be kwa DIAMOND PLATNUMS, amesema picha iliyotolewa kwenye gazeti moja la kila wiki akionekana bila nguo kuanzia kiunoni mpaka kichwani, iliibwa kwenye simu yake na mmoja kati ya marafiki zake.
Amesema hiyo picha ilikua kwa ajili ya mume wake mtarajiwa ambae ni DIAMOND, zaidi ya hapo hakua na nia nyingine yoyote na hiyo picha, lakini gafla akashtukia imesambazwa na kupelekwa kwenye gazeti.
hajaipeleka kwenye gazeti kama watu wanavyomsingizia, na wala hapendi kuanikwa hivyo kwenye magazeti……”nina ndugu zangu na watu wanaoniheshimu, hichi kitu kinaniharibia sana kuandikwa kiasi hicho, lakini kila kitu kinaenda na mazoea na inafikia point inabidi nikubali tu jinsi mambo yanavyokwenda” Wema aliiambia millardayo.com

No comments:

Post a Comment