kwa nje, kama ulimiss hizi picha za nje nilishazitoa kwenye millardayo.com zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Prof ameniambia hii nyumba alianza kuijenga mwanzoni mwa miaka ya 2000, na kiwanja alikinunua kutokana na shinikizo la MAREHEMU COMPLEX, aliemwamboa “bro we mtu kubwa sana sasa hivi, unapaswa kuwa na kiwanja na nyumba inayoendana na hadhi yako”mpaka sasa bado Prof hajapiga hesabu kufaham ni kiasi gani alitumia kujenga hii CRIB, lakini amekiri kwamba KAMA SIO UJANA wa MJINI, angekua ameimaliza siku nyingi sana, alikua anapata hela nyingi lakini hakuwezekeza kwa kishindo kama ilivyotakiwa, alinunua pia magari ya kifahari kama BENZ na BMW ambayo sasa hivi hayuko nayo tena.